Tuesday 16 September 2014

MIPANGO HAFIFU YA HALMASHAURI KARAGWE YALALAMIKIWA

Na
Juhudi  Felix
KAYANGA- KARAGWE
Baadhi ya abiria katika mji mdogo wa kayanga ,pamoja na wamiliki wa magari (daladala ) wamelalamikia uongozi wa halmashauri ya Karagwe kushindwa kutengeneza  miundo ya kuwepo kwa stendi ya wilaya  katika kipindi cha miaka 50 tangu wilaya ianzishwe
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Januari 23 mwaka huu baadhi ya abiria wameeleza kukerwa na magari ya abiria  na mizigo kujipanga  kandokando barabara  kutokana na stendi  jambo ambalo walisema linaweza kusababisha ajali
Mmoja wa abiria hao Selian Katabazi alisema utaratibu unaotumia wa kuegesha magari  kandokando ya barabara  ni hatari kwa maisha ya abiria
Alisema inashangaza kuona makao makuu ya wilaya  ambayo imeanza miaka 50 iliyopita  ikiwa tiyari inaongozwa na  na wakuu wa wilaya 21  na wakurugenzi 14 haina miundo  mbinu ya kuridhisha
Kwa upande wao wamiliki wa daladala  walieleza kusikitishwa na vitendo cha halamashauri  kuendelea kukusanya ushuru  katika stendi ambayo haikidhi vigezo
Walisema katika kikao cha bajeti  cha baraza la madiwani  wa halamashauri ya Karagwe  januari 15  mwaka huu  kilipanga vipaumbele 12  vya mpango wa bajeti  kwa mwaka 2014/2015  lakini hakuna bajeti iliyoelekezwa  katika ujenzi wa stendi  katika makao makuu ya mji huo
Mkurugenzi wa halamashauri Bosco Ndunguru  akijibu swali la diwani kata ya kayanga Adventina Kahatano CUF  alipotaka kujua kwa nini makao makuu hayana stendi ,alijibu kuwa itapangiwa bajeti katika mwaka ujao wa fedha na kukukiri kuwa katika vipaombele vya sasa bajeti hiyo haikutengwa

No comments:

Post a Comment