Thursday 18 September 2014

HARVEST ni nyumba ya wageni ya kisasa iliyofunguliwa wilayani Karagwe.

Harvest NI nyumba ya kisasa yenye mandhari mazuri ya kuvutia imefunguliwa wilayani karagwe mita  mia nne kutoka makao makuu ya wilaya kuelekea barabara ya omurushaka/Ngara ina Vyumba vya kisasa vyenye maji ya moto na Television yenye mtambo wa Dstv na ina Parking ya kutosha.Mkurugenzi wa Harvest anapenda kuwakaribisha wageni wote pindi mfikapo wilayani karagwe karibu upate huduma bora na ya kuridhisha,ina usalama wa kutosha,Ipo mita Hamsini kutoka barabara kuu na ina mazingira ya kutosha unayoweza kukaa na kupunga upepo. Karibu Karagwe Karibu Harvest.
 

















Kulia ni nyumba ya walinzi kwa ajili ya usalama wa wateja.








Tuesday 16 September 2014

WAKAZI WA TABORA WAKILI WAZI KUWA MASOKO NDIO CHANGAMOTO YAO KUBWA KATIKA SHUGHULI ZAO ZA UJASILIAMALI




SEMINA ya Kamata Fursa Jitathimini,Jiamini,Jiongeze inayoendeshwa sambamba na burudani za Fiesta 2014, jana imeendelea kwa kuwapatia dira ya maisha na namna ya kuwafanya wajikwamue kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi wakazi wa Mkoa wa Tabora mjini ndani ya ukumbi wa chuo cha TEKU,kilichopo katikati ya mji wa Tabora.
Semina hiyo ambayo imeongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa
Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (pichani juu) ilikuwa ya aina yake, kwani baadhi ya vitu na mbinu alizowapatia wakazi wa Mkoa wa Tabora,wengi wao wameonesha kuvutiwa nayo kutokana na mafunzo,maelekezo na mbinu mbalimbali za kupambana na changamoto zinazowakabili/zitakazowakabili katika miradi yao mbalimbali wanayotarajia kuianzisha ama wamekwishaianzisha.



 Mmoja wa Wajasiliamali kutoka mjini Tabora ,Dada Flora Zakaria ambaye amejiunga kwenye moja ya kikundi kinachofanya shughuli mbalimbali kupitia kikundi chao kiitwacho JACANA Natural Products,akionesha aina ya sabuni zilizotengenezwa na kikundi chao,ambapo pia kikundi hicho hujishughulisha na utengenezaji wa vipodozi vya asili kwa akina mama pamoja na mafuta ya aina mbalimbali.Flora alieleza kuwa wamekuwa wakijitahidi kutengeneza bidhaa mbalimbali lakini changamoto yao kubwa imekuwa ni namna ya kupata soko la kuziuza bidhaa zao.

 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha VETA wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikichambuliwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba (hayupo pichani).Ambapo washiriki wa semina hiyo waliunda vikundi na kubainisha wana miradi gani ama  wanatarajia kuanza kufanya miradi gani,ili kusaidia kutatua vikwazo na kutoa miongozo kwa namna moja ama nyingine.


 Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi,Mdau Mussa akizungumza na wakazi wa mjii wa Tabora waliofika kwenye semina ya Fursa,iliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha TEKU mjini Tabora.


 Sehemu ya Washirikiwa semina ya Fursa wakiwa ndani ya ukumbi wa Chuo cha TAKE wakifautilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo .

Ujumbe wa Jumuiya ya Africa Mashariki ukiwa eneo la Mtukula na ulipandisha bendera katika eneo hilo.






 

Wanafunzi wa shule za sekondari za wilaya ya Kyerwa,Missenyi na Ngara wapokea bendera ya Jumuiya ya Africa Mashariki.

 
 Wanafunzi   wa sekondari  wa shule ya wasichana  Baramba iliyopo wilayani  Ngara wakipandisha bendera ya Jumuiya ya  Africa  Mashariki.

 
Wanafunzi wa shule ya sekondari  ya  Bugene wakipokeaa   bendera ya jumuiya ya Africa Mashariki

Wanafunzi   wa Bunazi Sekondari iliyopo wilayani Missenyi wakiwa katika picha ya pamoja wakipokea  bendera kutoka kwenye jumuiya ya Africa mashariki

Hao wa ni wanafunzi  ni wa shule  ya sekondari ya Kaisho iliyopo  wilayani  Kyerwa ikumbukwe shule nne zimeteuliwa kutoa elimu ya hamasa juu

Ujumbe wa Jumuiya ya Africa Mashariki wakiwa katika ofis ya mkuu wa wilaya Missenyi


Wajumbe wakiteta jambo na  Mkuu wa wilaya ya Missenyi

Ujumbe kutoka   jumuia   ya Africa  mashariki wakiwa katika ofisi yaMkuu  wa wilaya ya Missenyi aliyekaa ni Mkuu wa Wilaya ya Missenyi Kanali Mstaafu Suleiman Issa  Njiku.
Add caption

Ujumbe wa Jumuiya ya Africa Mashariki wakiwa makao makuu ya Dayosisi ya Karagwe ya KKKT



 Ujumbe kutoka   jumuiya   ya Africa  mashariki wakiwa katika ofisi ya  Askofu wa KKKT  Dayosisi ya Karagwe Dk  Benson Kalikawe  Bagonza   mwingine ambaye yupo katika picha hizi ni Mkurugenzi wa Redio Fadeco Bw . Joseph Sekiku mwenye Skafu  shingoni.

Elimu ya uhamasishaji juu ya fursa zitokanazo na Jumuia ya Africa Mashariki kwa Wananchi Mkoani Kagera

Viongozi  wa Jumuiya  ya Africa  Mashariki wakiwa walivyotembelea shule ya sekondari Karagwe(KARASECO)  Picha  na Juhudi Felix wa FADECO redio.

 Wanafunzi  wa  shule ya sekondari ya karagwe wakiwa na  Bendera ya  Africa   Mashariki.

 Wakiwa wanafuatilia  kwa makini maelezo ya viongozi  hao