Ajali
hiyo ilitokea eneo la Mwanzo Mgumu kilometa moja kutoka mpakani mwa
Wilaya ya Bukoba na Wilaya ya Missenyi ambapo gari hilo aina ya costa
lilianza kutoa moshi mwingi kwa upande wa nyuma wakati likiwa kwenye
mwendo mkali na kuleta hofu kubwa kwa abiria walikuwemo ndani ya gari
hilo.
Mara baada ya dereva kugundua kuwa
gari analoendesha linataka kuungua alilisimamisha na kuwaambia abiria
wake kuwa gari linaungua.
Kwa
mujibu wa wabunge waliokuwemo kwenye gari hilo, baada ya kuambiwa kuwa
gari linaungua kila mmoja alifanya juhudi za kujiokoa, wengine wakipitia
madirishani.
Kwa Bahati hakuna Mbunge aliyeumia isipokuwa Mhe. Batenga aliumia mkono kidogo baada ya kubanana sana mlangoni.Baada ya kila mmoja kutoka gari hilo liliendelea kutoa moshi mzito sana lakini kwa halikushika moto na baadae lilizimika na kuacha kutoa moshi.
Wabunge
waliokuwemo katika gari hilo ni Rebbecca Mngondo (Arusha Viti Maalumu),
Rita Kabati (Iringa Viti Maalumu), Mariam Msabaha (Zanzibar Viti
Maalumu), Mhe. Batenga (Kagera Viti Maalumu), Mhe. Madabida (Dar es
Salaam Viti Maalum), Clara Mwatuka (Mtwara Viti Maalumu).
Wengine ni Mzee Hussein (Zanzibar),
Mussa Haji Kombo (Pemba Zanzibar), Abdul Mteketa (Jimbo la Kilombelo),
Mutula Mutula (Jimbo la Tunduru Kusini).Aidha Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Peter Serukamba Hakuwemo katika gari hilo lilotaka kuungua.
No comments:
Post a Comment