KAKONKO.
Wazazi wa wanafunzi wa shule ya msingi kihomoka ya
kijiji cha Kanyonza kata ya kakonko wilayani kakonko mkoani kigoma wamelaani vikali adhabu zinazo tolewa na
mwalimu mkuu wa shule hiyo Manyonyo
Stanley kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Kwa upade wake Mathayo Joseph amesema kuwa wamekuwa
wakiletewa malalamiko na watoto wao juu ya mwalimu huyo kuwatesa kwa kuwapiga
makofi na mateke badala ya viboko jambo ambalo ni ukiukwaji wa haki za watoto
na kinyume cha adhabu.
Akijibu malalamiko hayo mwalimu huyo amesema kuwa
yuko tayari kuwajibika kwa mzazi yeyote atakae fikisha malalamiko hayo kwa
mwajiri wake endapo kutakuwa na vielelelezo vya kutosha vitakavyo ridhisha kuwa
anatoa adhabu kinyume cha kanuni za adhabu kwa watoto wa shule za msingi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Yona Maki
amesema kuwa ofisi yakeimesikia malalamiko hayo na kwamba inaendelea kuyafanyia
kazi ilikujiridhisha na vitendo vya mwalimu huyo ili kumchukulia hatua za ki
nidhamu kwa mjibu wa kanuni za adhabu na utumishi.
Mwalimu huyo pia amelalamikiwa na mweyekiti wa
serikali ya kijijihicho kwa kumfukuza katika kikao cha kamati ya shule hiyo
kilichokukwa kikitarajiwa kuketi hapo 29Januari mwaka huu ili kufungua zabuni
za ujenzi wa chumba cha darasa ambapo mwlimu huyo amesema hamtambui mwenyekiti
huyo kama mjumbe halali wakamati hiyo.
No comments:
Post a Comment