Tuesday 16 September 2014

WAKAZI WA TABORA WAKILI WAZI KUWA MASOKO NDIO CHANGAMOTO YAO KUBWA KATIKA SHUGHULI ZAO ZA UJASILIAMALI




SEMINA ya Kamata Fursa Jitathimini,Jiamini,Jiongeze inayoendeshwa sambamba na burudani za Fiesta 2014, jana imeendelea kwa kuwapatia dira ya maisha na namna ya kuwafanya wajikwamue kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi wakazi wa Mkoa wa Tabora mjini ndani ya ukumbi wa chuo cha TEKU,kilichopo katikati ya mji wa Tabora.
Semina hiyo ambayo imeongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa
Clouds Media Group, Ruge Mutahaba (pichani juu) ilikuwa ya aina yake, kwani baadhi ya vitu na mbinu alizowapatia wakazi wa Mkoa wa Tabora,wengi wao wameonesha kuvutiwa nayo kutokana na mafunzo,maelekezo na mbinu mbalimbali za kupambana na changamoto zinazowakabili/zitakazowakabili katika miradi yao mbalimbali wanayotarajia kuianzisha ama wamekwishaianzisha.



 Mmoja wa Wajasiliamali kutoka mjini Tabora ,Dada Flora Zakaria ambaye amejiunga kwenye moja ya kikundi kinachofanya shughuli mbalimbali kupitia kikundi chao kiitwacho JACANA Natural Products,akionesha aina ya sabuni zilizotengenezwa na kikundi chao,ambapo pia kikundi hicho hujishughulisha na utengenezaji wa vipodozi vya asili kwa akina mama pamoja na mafuta ya aina mbalimbali.Flora alieleza kuwa wamekuwa wakijitahidi kutengeneza bidhaa mbalimbali lakini changamoto yao kubwa imekuwa ni namna ya kupata soko la kuziuza bidhaa zao.

 Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha VETA wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikichambuliwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kutoka Clouds Media Group,Bwa. Ruge Mutahaba (hayupo pichani).Ambapo washiriki wa semina hiyo waliunda vikundi na kubainisha wana miradi gani ama  wanatarajia kuanza kufanya miradi gani,ili kusaidia kutatua vikwazo na kutoa miongozo kwa namna moja ama nyingine.


 Mtangazaji wa Clouds FM kupitia kipindi cha Jahazi,Mdau Mussa akizungumza na wakazi wa mjii wa Tabora waliofika kwenye semina ya Fursa,iliyofanyika kwenye ukumbi wa chuo cha TEKU mjini Tabora.


 Sehemu ya Washirikiwa semina ya Fursa wakiwa ndani ya ukumbi wa Chuo cha TAKE wakifautilia yaliyokuwa yakijiri ukumbini humo .

No comments:

Post a Comment