Historia ya Wanyambo
Wanyambo ni kabila lilokuwa miongoni mwa makabila makubwa na yenye nguvu
za kivita na kiuchumi.Watu wa kabila hili la wanyambo walikuwa na
ufalme ulioongozwa na wafalme Abakama 14 kwa nyakati tofauti.Watu wake
ni wakulima na wafugaji.
Historia ya kabila hili ilifahamika ukanda wote wa Ziwa Magharibi
Victoria pamoja na nchi za Rwanda na Burundi.Kutokana na uhunzi wa
mapambo mengi ya kifalme yalitengenezwa na kuhifadhiwa kwenye ngome ya
mfalme.Mapambo hayo yalipendwa na mengine yalichukuliwa na Wajerumani
,walipewa zawadi na Omukama Rumanyika. Kwa ujumla ni kabila
lililoheshimika hivyo wanyambo walijivunia Unyambo wao hali iliyoibua
misemo kama, Ndyu Munyambo akala nakalenje, Omunyambo agamba echabweine.
Aidha anasema siku ya utamaduni wa Mtanzania ni utaratibu uliobuniwa na
Bodi ya Makumbusho ya Taifa chini ya Wizara ya Elimu na Utamaduni mwaka
1994 kabla Makumbusho ya taifa haijahamishwa chini ya Wizara ya
Maliasili na Utalii kama ilivyo sasa ili kutoa fursa kwa jamii
mbalimbali hapa nchini kuonyesha tamaduni zao katika Kijiji cha
Makumbusho ,Kijitonyama,Dar es Salaam.
 |
Nyumba za kiasili za wanyambo | | | | | | | | |
Wanyambo wengi hawajitambui
Inasemekana kwamba hata wanyambo wenyewe hasa waishio nje ya Karagwe
hawana ufahamu kama wao ni wanyambo au ni wahaya kwa sababu baadhi yao
hujitambulisha kama ni wahaya na wanajaribu hata kuigiza lugha yao.
Historia ya Wanyambo haijatafitiwa kwa kina na hivyo hakuna machapisho
ya kutosha yanayoelezea historia ya Wanyambo.Yapo machapisho machache
sana hasa ya Profesa Katoke na hadithi za wapelelezi kana Hans Mayer
ambayo hayako sokoni tena na yaliyopo hayatoshelezi mahitaji.
Anasema mila na desturi za Wanyambo zilizo nje ziko hatarini kutoweka
ikiwa ni pamoja na ngoma za asili, nyimbo ,misemo ,majigambo,hadithi na
taratibu za maisha nyingi zimetoweka na zilizobaki ziko hatarini kupotea
kabisa.
Mfano mzuri ni ngoma ya Amakondere ambayo imebaki ikichezwa na kundi
moja tu la wazee waishio Rwanyango ambazo hazijarekodiwa ambapo itakuwa
vigumu kurithishwa kizazi kimoja hadi kingine.
Aidha uwepo wa ngoma ile unategemea sana uhai wa wazee hao hata ala za
muziki wa ngoma hizo (Amakondere) hazilimwi tena na huenda mmea huu
umeshatoweka kabisa.Kwa upande wa lugha ya wanyambo (Orunyambo) imeanza
kupoteza uhalisia wake kutokana na mwingiliano na kutozungumzwa mara kwa
mara hivyo huenda ikapotea kabisa.
“Kwa ujumla wanyambo wanapata usumbufu katika kujitambulisha hasa
wanapohitaji baadhi ya huduma katika Wizara ya Mambo ya Ndani kwa sababu
hudhaniwa jamii ya wanyambo ni wakimbizi kutoka nchi jirani za Burundi
na Rwanda”.
hivi ndivyo tunaweza kutambulisha na kuendeleza kabila letu siyo kuwasindikiza wenzetu.pamoja tunaweza
ReplyDelete