SEMINA
ya Kamata Fursa Jitathimini,Jiamini,Jiongeze inayoendeshwa sambamba na
burudani za Fiesta 2014, jana imeendelea kwa kuwapatia dira ya maisha na
namna ya kuwafanya wajikwamue kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi
wakazi wa Mkoa wa Tabora mjini ndani ya ukumbi wa chuo cha TEKU,kilichopo katikati ya mji wa Tabora.
Semina
hiyo ambayo imeongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa
Clouds
Media Group, Ruge Mutahaba (pichani juu) ilikuwa ya aina yake, kwani
baadhi ya vitu na mbinu alizowapatia wakazi wa Mkoa wa Tabora,wengi wao
wameonesha kuvutiwa nayo kutokana na mafunzo,maelekezo na mbinu
mbalimbali za kupambana na changamoto zinazowakabili/zitakazowakabili
katika miradi yao mbalimbali wanayotarajia kuianzisha ama
wamekwishaianzisha.